Klabu ya Simba SC imetangaza kuachana na golikipa wake Beno Kakolanya, baada ya mkataba wake kumalizika klabuni hapo.
Taarifa ya klabu hiyo imesema:“Uongozi wa klabu unaujulisha umma kuwa hatutaendelea kuwa na mlinda mlango, Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika”
Wakati hayo yakijiri golikipa huyo amesema wazi kuwa tayari amepata ofa nono kutoka moja ya timu nchini.