Klabu ya Arsenal yarejea rasmi mazoezini

Washika mitutu wa London Arsenal Imeingia kambini tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2023|2024 wakiwa chini ya kocha wao Mikel Arteta.


Arsenal ambayo ilikuwa na msimu bora zaidi wa 2022/2023 baada ya kuongoza ligi kwa kipindi kirefu na kumaliza nafasi ya pili nyuma ya Manchester City huenda imeamua kuingia kambini mapema ili kurekebisha makosa yaliyoifanya kupoteza ubingwa mwishoni mwishoni kabisa mwa msimu huo.


Arsenal mpaka sasa imefanikiwa kuongeza nguvu katika kiosi chake kwa kumsajili Kai Havertz kutoka kwa majirani zao Chelsea na imekuwa ikihusishwa na usajili wa mchezaji Declan Rice kutoka West Ham United pamoja na Mastaa wengine kadhaa.


Aidha huenda mazoezi ya Klabu hiyo huenda yakaendelea bila uwepo wa Kiungo wake raia wa Uswizi Granit Xhaka (30) ambaye inaelezwa kwamba huenda atakamilisha uhamisho wa pauni milioni 21.5 kwenda Bayer Leverkusen ndani ya wiki hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *