Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Fredrick Shoo “Ileweke wazi kwamba Kanisa linaunga mkono uwekezaji unaofanywa Nchini licha ya kutambua kuna maoni mbalimbali kutoka kwa Wadau tofauti.
Kuhusu uwekezaji wa DP World ameongeza “Viongozi wa Dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona (Rais Samia) mwanzoni mwa jambo hili, kwa uungwana ukatupokea na tukakukabidhi maoni yetu na ukaahidi utayawasilisha kwa wataalam kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.”
Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT katika Chuo cha Tumaini Makumira Mkoani Arusha, leo Agosti 21, 2023.