Kizimbani kwa kumuomba rushwa mgonjwa ya Tsh Laki na nusu

Afisa Tabibu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba Msafiri Omary Kalomo, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Iramba, kwa shtaka la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh. 150,000 kutoka kwa Neema Msengi Kilimba ili amsaidie kufanya upasuaji wa uvimbe katika Tumbo la Uzazi.

Akisoma mashtaka katika kesi hiyo namba CC. 01/2024 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Luzango Khamsini, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU Wakili Yvonne Munisi, amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) & (2) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sura 329 Marejeo ya Mwaka 2022.

Hata hivyo, Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kesi imeahirishwa hadi Januari 18, 2024 ambapo mshtakiwa atasomewa hoja za awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *