KITUNDU APANDISHWA KIZIMBANI KWA SHAMBULIO LA AIBU TABORA

Kijana Ibrahimu Said maarufu kama kitundu, Aprili 17, 2026 amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tabora akituhumiwa kwa kosa la kumuingizia uume wake mdomoni mtoto wa kiume (6) jina limehifadhiwa, tukio ambalo anadaiwa kulifanya majira ya saa sita mchana katika mtaa wa Nyerere kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora.

Ibrahimu Said maarufu kitundu (18) katika shauri hilo la namba 8227 la mwaka 2026 anadaiwa kutenda kosa hilo la shambulio la aibu Marchi 22 mwaka 2026 katika mtaa wa Nyerere kata ya Ipuli manispaa ya Tabora baada ya kumchukua mtoto huyo nyumbani kwao na kwenda naye kwenye kibanda cha kurushia filamu ambapo akamdanganya na kumuwekea uume wake Mdomoni akimtaka aunyonye kwa ajili ya kujifurahisha kingono.

Katika maelezo ya awali ya kosa yaliyowasilishwa mahakamani hapo na wakili upande wa Jamuhuri Steven Mzava mtuhumiwa Ibrahimu Said maarufu kitundu anadaiwa kutenda kosa hilo la shambulio la aibu kinyume na kifungu namba 138 C (1) na (d) (2) (b) sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

Mbele ya hakimu katika mahakama hiyo ya wilaya Demetrio Nyakunga mtuhumiwa Ibrahimu Said maarufu kitundu alikana kutenda kosa hilo huku mahakama ikizuia dhamana kwa mtuhumiwa huyo kwa ajili ya usalama wake kutokana na kosa aliloshitakiwa nalo mahakamani hapo.

Hata hivyo shauri hilo limeahirishwa hadi tarehe 29 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena huku mtuhumiwa akipelekwa mahabusu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *