Mgombea Udiwani wa Kata ya Shinyanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Salum Kitumbo ameendelea kuinadi ilani ya chama cha mapinduzi (CCM), mara hii akifanya mkutano katika mtaa wa Kaunda uliopo kata ya mjini akiomba ridhaa ya Wananchi wamchague ili awe diwani wao, pamoja na kumpigia kura Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga, Patrobas Katambi, na kura za kishindo kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Sambamba na kufanya kampeni, Kitumbo pia ametumia jukwaa hilo kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Shinyanga Mjini, na kuahidi kuzitatua endapo wakimpatia ridhaa ya kuwa Diwani wao katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.

Amesema, kero mbalimbali ambazo zimewasilishwa na wananchiamezichukua na kama jukumu la kutekeleza kwake, na atakapofanikiwa kuwa Diwani wa Kata hiyo, ataanza nazo kama kipaumbele chake, ili Kata ya hiyo ipige hatua kubwa ya kimaendeleo.
Akijibu kero ya kutokamilika kwa uzio wa Shule ya Msingi Town,iliyopo katika manispaa ya Shinyanga amesema uzio huo endapo atafanikiwa kuwa diwani ataukamilisha, lakini kabla ya ujenzi wake ataangalia endapo sheria inaruhusu, ili wajenge Maduka kwa kuzunguka shule hiyo,ili wafanya biashara wapate sehemu ya kufanya biashara, pia shule ipate mapato na kuongeza mapato ya Halmashauri na taifa kwa ujumla.

Amejibu pia swali llilioulizwa katika mkutano huo kuhusina na mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halimashauri kwamba akiashaingia Halmashauri atahakikisha mikopo hiyo inapatikana kwa wahusika na kwamba atapambana fursa azote zilizopo katika halimashauri ya manispaa ya Shinyanga kiapumbele kiwe kwa wananchi wa kata ya mjini.
“Kero zote ambazo mmeziwasilisha kwangu na waombeni siku ya Uchaguzi Oktoba 29 mjitokeze kwa wigi mkanipigie kura ili nipate kuwa diwani wenu,mpigieni pia Patrobas Katambi, na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan,ili tuchape kazi kwa ushirikiano, umoja na kuwaletea maendeleo,” amesema Kitumbo.

Ahadi nyine amesema atahakikisha barabara zote za Kata ya Mjini zinawekwa Lami, Taa za Barabarani, kukamilisha ujenzi wa Soko Kuu la Shinyanga Mjini, pamoja na ajira zote ambazo zitakuwa zikitoka Halmashauri kipaumbele kitakuwa kwa vijana wa Kata hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdulaziz Sakala amesema Kata ya Shinyanga Mjini imepata Diwani ambaye ni Muadilifu, mchapakazi na anayependa kufanya mambo makubwa na kuwaahidi kuwa siku ya Uchaguzi Oktoba 29, wamchague Salum Kitumbo.



