KITUMBO AREJESHA FOMU UDIWANI KATA YA SHINYANGA MJINI

Na Eunice Kanumba- Shinyanga.

Salum Shabani Kitumbo amerudisha Fomu za uteuzi kugombea Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Kitumbo amerudisha Fomu hizo leo hii Agosti 27, 2025 kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi (INEC), Kata ya Shinyanga Mjini Simon Mashishanga, huku akisindikizwa  na wanachama wa Chama cha mapinduzi (CCM).

 Akizungumza mara baada ya kurudisha Fomu hizo, Kitumbo amesema anakishukuru Chama chake kwa kumuamini na kupitisha jina lake kugombea nafasi hiyo ya Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini,na kuahidi ataitendea haki katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha,ameomba makundi yote yaliyokuwapo wakati wa kura za maoni za kumtafuta mshindi mmoja wa kugombea nafasi hiyo ya udiwani,kwamba yavunjike na kuungana kuwa kitu kimoja na kutafuta kura za ushindi za chama cha mapinduzi katika ngazi za udiwani ubunge na urais.

Salum Kitumbo ni msomi mwenye  elimu ya shahada ya kwanza ya biashara na utawala kutoka chuo kikuu cha  Dar es salaam,na kabla ya kuingia katika mchakato huo wa siasa Kitumbo amekuwa  mshauri wa kibiashara  wa Makampuni ya  ya Jambo Group.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *