
NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA
KADA maarufu wa chama cha mapinduzi Salum Kitumbo amechukua na kurudisha fomu akitia nia kugombea udiwani wa kata ya mjini kwenye manispaa ya Shinyanga.
Kitumbo mweye elimu ya shahada ya kwanza ya bishara na utawala kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam lakini pia mwenye taaluma mbalimbali katika nafasi za uongozi huku akifanya kazi katika kada ya biashara ambapo amekuwa mshauri wa kibiashara wa kampuni ya jambo group of companies.
Kitumbo anatajwa kuwa ni miongoni mwa Wanachama wa muda mrefu wa Chama cha mapinduzi huku ikitajwa kuwa alijiunga na chama hiko tangu mwaka 1984.