Kitayosce wafungiwa

Klabu ya Ligi Kuu ya NBC, Tabora United ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama Kitayosce FC imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa mpaka itakapomlipa mchezaji Asante Kwasi.

Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo Raia wa Ghana kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo akidai malipo ya ada ya usajili na malimbikizo ya mshahara.

Mbali na uamuzi huo wa FIFA kuifungia klabu hiyo kufanya usajili, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia klabu hiyo kufanya uhamisho wa ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *