Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, limezinduliwa rasmi ili kuanza utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha 2025/2030 huku Diwani wa Kata ya Ndoleleji, Emanuel Limbe akichaguliwa kwa kura zote kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo na Diwani wa Kata ya Masanga, Enock Bundala akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Akizungumza katika kikao cha kwanza cha baraza hilo, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Kishapu, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Peter Masindi amewataka madiwani hao kuvunja makundi na badala yake wakasikilize na kutatua kero za wananchi.

Amesema, Wananchi wana imani na madiwani hao na ndiyo maana waliwachagua ili wakawatumikie, hivyo wanatakiwa kuwafikia wananchi kwa haraka katika maeneo yao na kutatua changamoto zao kwa wakati, pamoja na kujiepusha na maslahi binafsi katika miradi mbalimbali ya Serikali itakayoletwa katika Kata zao.
DC Masindi pia amewataka walioapishwa kwenda kumaliza tofauti za kisiasa udini a ukabila katika maeneo yao pamoja na kuwalinda na kushrikiana na watumishi wa Serikali pasipo kuleta migogoro baina yao, ili utekelezaji wa majuku ya kuwadumia wananchi kwa weledi na uafanisi.

“Nendeni site mkakutane na wananchi waliowapa kura lakini pia mkahakikishe miradi ya maendeleo inaenda kwa wananchi na inatekelezeka kwa wakati,” amesema DC Masindi.
Kwa upande Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Josephat Limbe akitoa neno la shukrani baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa halimashuri hiyo amesema wanachi katika wilaya ya Kishapu wanaitaji maendeleo pamoja hivyo atashirikiana kwa dhati na viongozina wataalamu katika halimashuri kuhakikisha kila kinatekelezeka kwa weledi

Limbe amesema Wialya ya Kishapu ina Kata 29, Vijiji 117 na Vitongoji 660, hivyo ni eneo kubwa kijiografia lenye kuhitaji utulivu wa hali ya juu katika kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba Madiwani wakatekeleze pia yale waliyohaidi katika kipindi cha kampeni.
“Mimi binafsi Ninaamini katika mashirikiano hivyo twendeni tukashirikiane na wananchi lakini tukasimamie maelekezo ya Mheshimiwa Rais na yale tutakayokuwa tumekubaliana katika baraza letu,” amesema Limbe.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Emmanuel Johnson amewataka madiwani hao hususan wale ambao ndiyo wameingia kwa mara ya kwanza katika baraza hilo kusoma kanuni na miongozo ya baraza la madiwani ili kutekeleza majukumu yao kwa mujibu kwa uadilifu na uwazi.
Jambo media pia imeafanikiwa kizungumza na baadhi ya madiwani waliopishwa kuanza majukumu yao akiwemo Diwani wa Kata ya Bubiki, James Kasomi amesema Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa mno na madiwani hao hivyo wankwenda kurejesha matumani kwa kushughukikia miradi ya barabara zahanati pamoja na changamoto nyingine.

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalumu kutoka Kata ya Ukenyenge, Sophia Julius Masele amesema mara tu baada ya kuapishwa wanawahaidi wananchi kutimiza yale yote waliyohaidi katika kipindi cha kampeni kupitia kamati za kisekta na za kudumu za baraza la madiwani walizounda hivyo kwa ushirikiano wa pamoja wilaya ya Kishapu itasonga mbele.


