Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kisa Yanga aliachwa na mpenzi wake

Msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara, Feisal Salum ‘Fei Toto’ alikuwa akikipiga Yanga na pakatokea sakata la kuondoka klabu hiyo na hatimaye akaijiunga Azam FC.

Kwa mujibu wa gatezi la Mwananchi, kiungo huyo matata anafunguka sakata lakuachwa na mpenzi wake kisa tu kuachana na Yanga SC.

“Lile sakata liliniathiri kwenye mambo mengi sana sio kwa upande wa kucheza pekee, wakati niko kwenye wakati mgumu kama ule kila wakati unafikiria hii kesi itaishaje, nikakutana na pigo lingine la kukimbiwa na mpenzi wangu ambaye niliamini ningekuja kumuoa.

“Aliona kama maisha yangu ya soka tena basi ndio yameishia pale alishindwa kuvumilia na kuamua kutafuta mtu mwingine kitu kilichoniumiza zaidi ni hatua mbaya zaidi kwangu ikawa kwenda kuolewa tena nikiwa katikati ya lile sakata, sikuwa nimemuoa ila tulikuwa na mipango mingi ya maisha kati yetu, hakutaka kuvumilia kabisa nililazimika kuyapokea maamuzi yake hakukuwa na namna na sasa nimerudi uwanjani maisha mengine yataendelea tu.”

#Chanzo:Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *