Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi, Jamila Yusuf ametoa maelekezo ya kufungwa kwa shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu katika migodi ya Lumuka iliyopo Kijiji cha Dirifu kutokana na watu 17 kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa kupindupindu.
Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Wilaya kutembelea maeneo ya migodi leo, Januari 6, 2025 na kukuta watu wanaofanya shughuli kwenye eneo hilo la mgodi zaidi ya 3,000 wakiwa hawana vyoo na badala yake wanajisaidia vichakani.
DC Jamila amesema “Niwape pole wananchi wa hapa Lumuka mnaofanya kazi katika machimbo haya kwa wenzenu 17 kugundulika na maambukizi ya kipindupindu. Idadi hii ni kubwa sana’ – DC Jamila
“Serikali inawapenda na inawajali wachimbaji wakubwa, wakati na wadogo, lakini haiko tayari kuona wananchi wake wanaathirika au kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huu wa kipindupindu. Kwanza ni aibu watu zaidi ya elfu tatu kukosa vyoo na mnajisaidia vichakani’ – DC Jamila.
Baada ya kumaliza kukagua DC Jamila akasema “Nafunga shughuli zote katika maeneo haya ya migodi mpaka mtakapokamilisha ujenzi wa vyoo vya kisasa ndani ya siku saba viwe tayari, ili muendelea na shughuli zenu vinginevyo hatutaruhusu uchimbaji uendelee hapa,” – DC Jamila.
Contact Us
P. O. BOX 71, Shinyanga, Tanzania
+255 766 408 253
info@jambofm.co.tz