Kiongozi na muimbaji wa Kundi la Morgan Heritage amefariki Dunia

Kiongozi na muimbaji mkuu wa Kundi la Morgan Heritage Peter Morgan (Peetah) amefariki Dunia. Ingawa kwenye taarifa ya familia ya Morgan Heritage hawajasema chanzo cha kifo.

Kwenye post waliyopost Morgan Heritage wameandika ‘kwa upendo wa dhati tunatangaza, mume, baba, mwana, na kaka na mwimbaji mkuu wa Morgan Heritage Peter Anthony Morgan amefariki Dunia leo Februari 23″ 2024’

‘Familia yetu inakushukuru kwa upendo wenu mwingi, na tunakushukuru kwa maombi yenu tunapopitia mchakato huu. Pia tunaomba uheshimu faragha yetu wakati huu wa msiba. Asante!’ – Familia ya Morgan.

Peter wa Morgan Heritage alifanikiwa kushirikiana baadhi ya kazi na Wasanii kutoka Tanzania kama Harmonize, Diamond na Rommy Jones.

Peter Morgan amefariki akiwa na umri wa miaka 46.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *