KINYWAJI CHA JAMBO MWAMBA CHAZINDULIWA RASMI

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Kampuni ya Jambo Group imezindua rasmi kinywaji  chake kipya kinachojulikana kwa jina la Jambo Mwamba.

Uzinduzi huo umefanyika leo, Juni 7, 2025, katika Viwanja vya Zimamoto vilivyopo jirani na Soko la Nguzonane, ndani ya  halimashuri ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Kiongozi Mkuu wa Jambo Media, ambaye pia ni Kiongozi wa Ubunifu na Msimamizi wa Chapa wa Jambo Group, Nickson George, amesema kuwa bidhaa hiyo ni ya kipekee na imelenga kuwawezesha vijana kupata hamasa, kujiamini,na kuonyesha vipaji vyao kwa ujasiri.

“Kampuni ya Jambo Group tumekuwa tukifanya matamasha mbalimbali pamoja na kampeni maalum kwa ajili ya kuibua na kukuza vipaji vya vijana, kupitia uzinduzi wa bidhaa zetu, leo tumezindua kinywaji kipya cha Jambo Mwamba,”amesema George.

 Aidha Nickson ametoa wito kwa vijana kuendelea kushiriki katika matamasha mbalimbali yanayoandaliwa na kampuni  ya Jambo Group  ili kuendeleza na kutangaza vipaji vyao, huku akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia kufanikisha ndoto zao.

Kwa upande wao baadhi ya vijana walioshiriki kwenye tamasha hilo la uzinduzi, wameishukuru Jambo Group kwa kuendelea kufanya majukwaa ya kuonyesha vipaji, wakieleza kuwa hiyo ni nafasi ya kipekee ambayo imekuwa chachu ya maendeleo yao.

Katika tamasha hilo, vipaji mbalimbali vilionyeshwa ikiwa ni pamoja na kuimba, kucheza, kupiga danadana, pamoja na kushiriki mashindano ya kula ugali,mikate, na kuvuta kamba.

Uzinduzi huo ulipambwa na burudani ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya Dvoice kutoka katika lebo ya WCB Wasafi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *