Kinara madawa ya kulevya nchini akamatwa

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imemkamata kinara wa mtandao wa Wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina cocaine nchini pamoja na kukamata jumla ya gramu 692.336 za cocaine zinazowahusisha Watuhumiwa wanne katika operasheni maalum zinazoendelea Nchini.

Mfanyabishara huyo wa mtandao wa cocaine ambaye alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu amekamatwa katika eneo la Boko Jijini Dar es Salaam pamoja na washirika wake watatu ambapo kati yao wawili walikamatwa jijini Dar es Salaam na mmoja alikamatwa katika kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini Mkoani Mbeya.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo akiongea leo Jijini Dar es salaam amesema Mamlaka imebaini Wafanyabiashara wa matandao wa cocaine wamekuwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia Watu ambao humeza dawa hizo tumboni au kuweka

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *