KINACHOWEZA KUZUIA UCHAGUZI USIFANYIKE NI VITA PEKEE – DEVOTA MINJA

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Devotha Minja amesema kitu pekee kinachoweza kuzuia uchaguzi usifanyike ni uwepo wa vita na si matamko au maandamano.

Devota ameyasema hayo hii leo Mei 21, 2025 jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kinyume na hapo hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi kwa namna yoyote na kuwataka wana CHAUMMA kuingia kwenye mapambano.

Amesema, “twendeni tushiriki uchaguzi huu tukapiganie mabadiliko ambayo tunaamini tutayapata tukiwa ndani ya uwanja huu. Na kamwe hatuwezi kushinda vita tukiwa nje ya ulingo na hatuwezi kuchukua kombe kama tumeondoa timu uwanjani.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAUMMA Taifa, Hashimu Rungwe amesema Taifa ambalo halina lishe, halitaweza kuendelea, ndio maana wanaamini ili kujenga taifa madhubuti na lenye watu imara, ni lazima kuhakikisha watu wanapata lishe madhubuti tangu wakiwa watoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *