Baada ya baba mtoto, Brown Mauzo, kuachia picha inayoonyesha sura ya mtoto wake Ice Brown, Mama mtoto Vera Sidika amelazimika na yeye kuachia picha ya kijana wake huku akimtakia kheri ya miezi saba ila ameweka wazi kuumizwa na kitendo cha mzazi mwenzake kuachia picha bila ridhaa yake.
“Mungu amenibariki na mtoto mzuri wa kiume @prince_icebrown 💙 Ni furaha kwangu kuona pia ana afya mtoto wangu, lakini pia naahidi kuwa nitatoa kila kitu ndani yangu ili kuhakikisha kuwa maisha yake yatakuwa bora zaidi. Heri ya miezi 7 @prince_icebrown 💙 N.B (ilibidi tu, nitoe picha hii ya kuonyesha uso wake maana picha imetolewa bila hata kunijulisha 🤦♀️