Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza mkoani Kigoma, Zainab Mbunda na Mweka Hazina wa Halmashauri hiyo Majid Mabanga ili kupisha uchunguzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), kwa madai ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo tayari Serikali imekwishatoa fedha.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa uamuzi huo mkoani Kigoma mara baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uvinza na jengo la halmashauri hiyo ambayo licha ya Mkurugenzi kukiri kuwepo kwa fedha za utekelezaji wake toka mwaka 2021 ujenzi wake bado haujakamilika.