Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesema anaunga mkono maamuzi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin ikiwa ni pamoja na operasheni yake ya kijeshi nchini Ukraine.
Kim amesema wakati wawili hao walipokutana nchini Urusi kuwa “Korea Kaskazini inaunga mkono maamuzi yote ya Putin,” amesema akiongeza. “Urusi imeibuka katika mapambano kulinda mamlaka yake na usalama dhidi ya vikosi vya kivita.