KILELE WIKI YA POLISI JAMII SIMIYU CHAWAFIKIA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Na Saada Almasi, Bariadi – Simiyu.

Kwa mara ya kwanza jeshi la Polisi limeadhimisha wiki ya Polisi Jamii katika maeneo mbalimbali nchini, kama ishara ya kuendelea kujisogeza karibu na jamii, ili kuboresha mahusiano.

Katika maadhimisho hayo ambayo yamepambwa na matendo ya huruma, Jeshi hilo mkoani Simiyu likiongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP). Asiago Ochieng limetoa elimu ya Usalama Barabarani katika shule ya Msingi Somanda A Mjini Bariadi, pamoja na kutoa zawadi kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Akiongea Shuleni hapo, Kamanda Ochieng amesema, “ni vema tukajenga uhusiano mzuri kati ya Jeshi la Polisi na Jamii yetu kwa kuwa yapo maeneo ambayo yanahitaji kuguswa na kila mtu, ukiangalia hapa wapo watoto wanaotuhitaji kwa kuwa tunajiweza, hivyo tunapokuwa karibu nao hawatojiona kuwa wanatengwa.”

Aidha, amewataka Wanafunzi kutosita kutoa taarifa yoyote ambayo wanamashaka nayo katika maeneo wanakoishi, kwa kupitia njia sahihi kama kuwaambia walezi wao ama Polisi walio karibu nao.

Kilele cha wiki ya Polisi Jamii kitakuwa kikifanyika Agosti 25 ya kila mwaka ambapo Polisi watashiriki shughuli mbalimbali za kijamii, sambamba na kufanya matendo ya huruma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *