Simba imepangwa kukutana na Al Ahly ya Misri wakati Yanga ikiangukia mikononi mwa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini katika michezo yao ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, na wote wawili wataanzia nyumbani.
Mechi za mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Machi 29-31 na kurudiana kati ya Aprili 5-7, 2024.