KILA MTANZANIA ANA WAJIBU WA KUULINDA MUUNGANO – DKT. TULIA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DkT. Tulia Ackson amesema ni wajibu wa kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha anaulinda Muungano.

Ameyasema hayo hii leo Aprili 25, 2025 Mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Amesema, “Tanzania haiwezi kuwepo bila Muungano, Muungano huu umejengwa katika misingi imara umedumu na utaendelea kudumu. Kila mmoja wetu anapaswa kutafakari matendo na maneno yake yawe chachu ya kudumisha Muungano.”

“Niwahakikishie kwamba Bunge litaendelea kuwa daraja katika pande zote mbili ili kuhakikisha Muungano unazidi kuwa madhubuti, unadumu na kuwa imara zaidi,” alisisitiza Dkt. Tulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *