Kila kidole unachovaa pete kina maana

Siku hizi suala la kuvaa pete kama urembo limekuwa la kawaida na kila mtu anavaa na linamvutia kutokana na kuwa anapendezesha muonekano wake.

Ila kupitia stori hii nakujua kuhusu kila kidole utakachovaa pete kina maana gani?

Ukivaa pete kidole gumba ina maanisha una mali na pia una afya njema.

Kidole cha pili kutoka gumba ukivaa pete kinaashiria uongozi au cheo katika jamii.

Siku ukimuona mtu kavaa pete kidole cha kati jua huyu ni jasiri lakini yupo kwenye harakati za kutafuta mweza wake.

Usije kujichanganya hapa siku ukiona mtu amevaa pete kwenye kidole cha nne kutokea gumba, huyu anakuwa ameoa au kuolewa.

Na anayevalia pete kidole cha mwisho (kidogo) ishara kuwa huyu ni mtu anaye jali familia,ana akili na muwaminifu sana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *