Kikao chafanyika kunusuri Kurugenzi FC

Timu ya Kurugenzi FC ya Maswa mkoani Simiyu (101.5 Jambo FM), inayoshiriki ligi daraja la pili Tanzania bara (First League), ipo katika nafasi mbaya kwenye msimo wa ligi hiyo, ikishika nafasi 6 Kundi B lenye jumala ya timu 8.

Hali hiyo imewashtua wadau wa mchezo mpira wa miguu mkoani Simiyu, ambapo hii leo chama cha soka Simiyu (SIFA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Bw. Osuri Kosuri, kimefanya kikao kizito na Viongozi wa timu hiyo kujadili mustakabali wa timu hiyo hasa kuelekea kuanza Kwa duru la pili Februari 02.

Ambapo pia, siku ya Alhamis chama cha soka, viongozi wa timu pamoja na wadau wengine watafanya kikao na Katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo kupanga mikakati ya namna gani wanaweza kuinusuru timu hiyo inayoshiriki ligi hiyo kwa takribani misimu minne sasa, isishuke daraja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *