Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kuwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa wastani inalaza wagojwa wa kiharusi 20 kwa kila mwezi ambapo kuanzia mwezi februari mpaka juni mwaka huu wagonjwa 108 wamegundulika kuwa na kiharusi huku ikielezwa kuwa watu walio na umri chini ya miaka 45 wako hatarini zaidi kupata ugonjwa huo.
Akizungumza mara baada ya kutoa elimu kwa watumishi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dkt John Luzila amesema wameamua kutoa elimu hiyo kutokana na ukubwa wa tatizo linavyoongezeka katika jamii, huku akiyataja baadhi ya magonjwa yanayopelekea kupata ugonjwa huo.
Baadhi ya watumishi wa hospital hiyo wamesema elimu waliyoipata itawasaidia kuhakikisha wanajikinga na baadhi ya mambo yanayopelekea kuugua ugonjwa huo na kwamba watashiriki kikamilifu kutoa elimu kwa jamii juu ya kutembelea vituo ya afya mara kwa mara.