Tume ya haki za Binadamu na Utawala bora nchini imeanza kutoa elimu ya Utawala Bora kwa Wananchi Mkoani Kigoma ikiwa ni Mkakati wa Serikali wa kuhakikisha wananchi wanazifahamu haki zao, ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji hususani kwa wananchi wa hali ya Chini.
Akizungumza wakati wa Mafunzo kwa watendaji wa Kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Kamishina wa Tume hiyo, Amina Twaribu Ally amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwaimarisha watendaji hao ili waweze kutoa haki katika Jamii.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/Screenshot_20250213-184051_PixelLab.jpg)
Kwa upande wao baadhi ya watendaji waliopata Mafunzo hayo akiwemo mtendaji wa kata ya Kitongoni Ramadhan Kalukura amesema mafunzo hayo yamewakumbusha wajibu wao hususani katika suala la Utawala Bora.
Tume hiyo inatarajia kutembelea wilaya zote za Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kutoa elimu hiyo kwa wananchi vyuoni shuleni na kwa viongozi mbalimbali.