KIFO CHA MTOTO KISIMANI TABORA: WAZAZI KUWENI WAANGALIFU – SACP ABWAO

Na Pascal Tuliano – Tabora.

Mtoto Ramin Sahbdad (3), Mwanafunzi wa Shule ya Mother Care na mkazi wa Kata ya Mpela iliyopo Manispaa ya Tabora, amekutwa amekufa maji kwenye kisima kilichopo nyumbani kwao.

Taarifa ya tukio hilo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao ambapo amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2025.

Amesema, mtoto huyo alikuwa anacheza karibu na kisima kilichopo ndani ya nyumba hiyo wakati mama yake akiendelea na kazi zingine za nyumbani.

Hata hivyo, taharuki ilitanda kwa mama yake baada ya kumkosa mwanaye, mpaka pale alipogundulika na jirani yao aliyekuta mwili wa mtoto huyo ukielea juu ya maji kwenye kisima hicho.

“Tarehe 20/07/2025 aligundulika akionekana akiwa anaelea juu ya maji ya kisima baada ya jirani yao aitwaye Agness Mageni kwenda kuchota maji katika kisima hicho,” alisema Kamanda Abwao.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoani humo limetoa wito kwa wazazi na walezi kuwa wangalifu dhidi ya Watoto wao wanapocheza kwenye maeneo hatarishi kama visima, ili kuepukana na matukio ya aina hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *