Wanafunzi wa kidato cha nne wameanza Mtihani wa taifa leo Novemba 13 2023 ambapo jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya Mtihani huo ni 572,338, kati yao watahiniwa wa Shule ni 543,386 na watahiniwa wa Kujitegemea ni 28,952 katika shule za Sekondari 5,371 na Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 1,798.
Aidha jumla ya Watahiniwa wa Shule wenye mahitaji maalum ni 614 na Watahiniwa Nane wa kujitegemea, ambapo wanafunzi hao wanatarajia kumaliza mtihani huo Novemba 30, 2023.
Jambo Fm inawatakia kila la heri.