KESI YA UHAINI: LISSU ADAI UTARATIBU WA MAHAKAMA UNACHEZEWA,HAKIMU ATAJA TAREHE

Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imeahirishwa hadi Julai 30, 2025.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi hiyo baada ya Jamhuri kuomba ahirisho, ili kusubiri maamuzi ya Mahakama Kuu juu ya maombi ya kuwaficha mashahidi.

Awali, Lissu alidai upande wa mashtaka unaficha ushahidi wa kesi hiyo ya uhaini na kusema hatoomba huruma ya Mahakama akitaka utaratibu usichezewe.

“Mimi siombi huruma ya mahakama, na sijaomba na sitaomba. Ninachotaka ni kwamba utaratibu wa mahakama usichezewe,” alisema Tundu Lissu.

Aidha ameongeza kuwa, Mawakili wa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wanachezea utaratibu wa Mahakama, jambo ambalo ni kinyume na wajibu wao wa kikatiba.

Katika kesi hiyo ya uhaini ambayonimesikilizwa mubashara kupitia ukurasa rasmi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Lissu ameeleza ahirisho la mara kwa mara la kesi hiyo ni mfano wa matumizi mabaya ya mchakato wa Mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *