Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kesi ya Marioo yasogezwa mbele hadi Mei

Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya, Arusha imeahirisha shauri la msanii wa muziki nchini, Marioo na Meneja wake Sweetbert Mwinula, hadi Mei 6, 2024 . Wawili hao wanadaiwa zaidi ya Tsh/=Milioni 500 kwa kuvunja makubaliano ya mkataba.

Shauri hilo liliahirishwa kwa sababu Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza shauri hilo hakuwapo mahakamani na mdai alifika mahakamani, ila wadaiwa hawakufika mahakamani.

Marioo alifunguliwa kesi na Kampuni ya Kismaty kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza kwenye hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu kanda ya Kaskazini Septemba 23, 2021 na wanakabiliwa na madai ya TZS Milioni 500. Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa Machi 18 na 19, mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *