Kesi ya uhaini Namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imeahirishwa hadi Februari 11, 2026.
Kesi hiyo, iliendelea hii leo Februari 9, 2026 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam ikisikilizwa na jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru.
Upande wa Jamhuri hii leo ulijibu hoja za mapingamizi yaliyowekwa na mshtakiwa Novemba 12, 2025 ilipotajwa kwa mara ya mwisho Mahakamani hapo.

Msingi wa mapingamizi hayo unatokana na shahidi wa siri wa Jamhuri (PW11) na kizimba cha siri cha kuongelea shahidi kilichopo kwenye chumba cha Mahakama
Baada ya Mahakama kusikiliza hoja za pande zote mbili, kesi hiyo aikaahirishwa hadi tarehe hiyo, kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa mapingamizi, ili kuendele na ratiba zinazofuata.