KESI YA LISSU, UCHAGUZI MKUU 2025: BUNGE LA ULAYA LATAKA HAKI ITENDEKE

Bunge la Ulaya (EU) limetoa maazimio sita kwa Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, huku likitaka haki itendeke kwenye kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Katika azimio hilo, wametaka Kesi ya Lissu kuendeshwa kwa uwazi, Mamlaka za Tanzania kulinda uhuru wa kisiasa, usalama wa waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu, na CHADEMA kuruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Aidha, Wabunge hao pia wamelaani kitendo cha kukamatwa kwa Tundu Lissu pamoja na tuhuma zinazomkabili, ambazo wanasema zinaonekana kuwa za kisiasa na zinazobeba hatari ya kifo.

Wametaka pia Sheria za uhalifu wa mtandaoni na vyombo vya vyaari vya Tanzania kuzingatia sawa na zile za kimataifa za haki za binadamu, kuheshimu haki za vyama vya siasa na kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.

Aidha, wanaitaka Tanzania pia kufuta hukumu ya kifo na kubadilisha hukumu zote za kifo, huku wakisisitiza haja ya EU kuhakikisha ushirikiano wake wa kimaendeleo na Tanzania, ikiwa ni pamoja na mpango wa Global Gateway, unaendana na uendelezaji wa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na viwango vya kesi vyenye haki.

Wabunge hao wanamuagiza Rais wake kupeleka azimio hilo kwa Serikali na Bunge la Tanzania pamoja na Umoja wa Afrika, azimio ambalo linatarajiwa kupigiwa kura na wabunge hao hii leo Mei 8, 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *