Mahakama Kuu ya Mkoa wa Iringa Chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta, leo Februari 1, 2024 imesikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Maria Ngoda dhidi ya jamhuri.
Akiongoza jopo la mawakili upande wa mkata rufaa, Wakili Moses Ambwindile amesema leo wametetea sababu zao za Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi.
Aidha Jaji Mgetta ameahirisha shauri mpaka kesho Februari 2, 2024.
Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3, 2023.
Kesi ya aliyekutwa na vipande 12 vya swala na kuhukumiwa Miaka 22 yaanza kusikilizwa