Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kesi 105 za ukatili zimeripotiwa Mkoa wa Shinyanga

Jumla ya kesi 105 za ukatili zimeripotiwa dawati la jinsia Mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha kuanzia Januuari 2023 hadi Desemba 1,2023 huku idadi ya matukio yaliyoripotiwa ikiongezeka tofauti na mwaka 2022 kutokana na jamii kuwa na uelewa wa utoaji taarifa.

Akizungumzia matukio hayo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Acp Janeth Magomi amesema kuongezeka kwa idadi ya matukio yaliyoripotiwa kumechangiwa sana na elimu inayotolewa na mtandao wa Jeshi la Polisi Wanawake Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu.

Nao baadhi ya wananchi na wadau wa haki za binadamu wamesema serikali imekuwa ikishirikiana kukomesha matukio hayo hali iiliyopelekea jamii kuondokana na uoga katika suala zima la utoaji wa taarifa pindi wanapofanyiwa vitendo vya ukatili.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili ilianzishwa na katibu mkuu mstaafu wa umoja wa mataifa Kofii Anan mwaka 2006 lengo likiwa ni kuitaka dunia itambue kuwa lipo tatizo kubwa la ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake na watoto hvyo kampeni hiyo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 25 Novemba hadi Disemba 10 kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *