Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kayumba adai kutapeliwa na mfanyakazi wa Rayvanny

Msanii wa muziki nchini, Kayumba amefunguka kuzulumiwa na Director Elly Mzava ambaye anafanya kazi na Rayvanny chini ya Next Level Music, kwa kile alichodai kuwa mwaka 2023 alitoa ngoma ya ‘Shake’ akimshirikisha Rayvanny inayopatikana kwenye Albamu yake ya FINE TAPE na alitakiwa kutoka Milioni 7 iliaweze ku-shoot video nzuri ila sivyo ilivyokuwa.

Kayumba ameenda mbali kwa kuweka chati alizochati na uongozi wa Next Level Music akiomba pesa yake irudi na pia ameomba msaada serikali kuweza kupata haki yake.

MIMI NI MOJA KATI YA WASANII WANAOPAMBANIA NDOTO ZAO WENYEWE USIKU NA MCHANA PASIPO KUWA NA LABEL YOYOTE APA TZ. NI MUNGU, MEDIA NA FANS WANGU WANAPENDA MZIKI WANGU NDO WANAOFANYA NIWEPO MASIKIONI MWA WATU MPAKA LEO .

LEO NTAWAAMBIA KITU AMBACHO HAMJAWAHI KUKIIJUWA NA NITAWAAMBIA KWANINI NIMEWAPOST HAWA WAWILI.

👉 MNAMO MWEZI WA PILI MWAKA JANA NILIKUWA NA PROJECT YANGU YA ALBUM ILIYOITWA ( FINE TAPE ) HUMO NDANI KUNA COLLABORATION KADHAA IKIWEPO #SHAKE NILIOMSHIRIKISHA NDUGU YANGU @rayvanny NA KWENYE COLLABO HIO NILIPASWA KUTAFUTA M.7 AMBAYO NILIAMBIWA NA NDUGU DIRECTOR ELLY MZAVA AMBAYE YEYE NDO ATAKAE SHOOT VIDEO HIO .
NILIMTAFUTIA MZAVA M 7 NA NIKAMKABIDHI NDANI YA OFFICE ZA @nextlevelmusic_tz MBEZI BEACH KWA KUAMINI NITAPATA KITU KIZURI CHA KUWAPA FANS WANGU . LAKINI HAIKUWA IVYO

BADALA YAKE MIZUNGUSHO IKAANZA BAADA YA KUWAPATIA PESA NA ILE VIDEO TULIOKUBALIANA HAIKUFANYIKA MPKA LEO HIII , NA PESA YANGU WAKACHUKUA PASIPO KUANGALIA KUWA MI NI KIJANA MDOGO TENA NINAEPAMBANIA NDOTO ZANGU KWA NGUVU ZOTE 😭😔😭,

LAKINI SIKUCHOKA NIKAJARIBU PIA KUWATAFUTA UONGOZI WA RAYVAN NA NIKAONGEA NAO MARA KADHAA LAKINI JITIHADA ZANGU HAZIKUZAA MATUNDA NA NIKAONEKANA MI MSUMBUF KWA KUDAI HAKI YANGU MNYONGE MIMI😔

SASA NIMEONA NIPOST HAPA KWENYE INSTA YANGU SIO KUWADHALILISHA HAPANA.
ILA NIMEFANYA IVI FANS WANGU MULIFAHAM KUWA NIMEZURUMIWA LAKINI PIA SERIKALI YA MMA ANGU @samia_suluhu_hassan NAOMBA WALIANGALIE HILI KAMA KUNA MSAAADA WOWOTE WA MI KUPATA HAKI YANGU BAS NISAIDIWE AU TUSHIKANE MASHATI MAANA NIMEVUMILIA VYA KUTOSHA KUSUBIRI HAKI YANGU SIIPATI.🤨🤬😭

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *