Mashabiki wa mwimbaji wa Marekani Jason Derulo wameoneshwa kutopendezwa na picha ya albamu yake ya “Nu King” aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha amevalia taji la miiba wakidai kuwa anamdhihaki na kumkufuru Yesu Kristo.
“Another one mocking Jesus! Show respect!” Amesema shabiki mmoja.