Waziri wa kilimo Hussein Bashe amesema serikali imeruhusu kuingizwa kwa tani laki moja ya sukari toka nje kutokana na hali ya uzalishaji wa viwanda vya ndani kuathiriwa na mvua kubwa za El-nino zinazoendelea kunyesha.
Bashe ameyasema hayo leo tarehe 20 Januari, 2024 jijini Dodoma, ambapo amesema hali ya bei ya sukari itakayoendelea kuimarika itarejea katika utulivu katikati ya mwezi Februari huku akiyataka makampuni kuhakikisha hayafichi sukari au kuruhusu kupaa kwa bei kwa gharama ya Mlaji.