Afisa Habari wa Klabu ya Soka ya Yanga SC, Ally Kamwe anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora, kwa tuhuma za kutoa kauli mbaya dhidi ya Viongozi wa Serikali.
Taarifa za kukamatwa kwa Ally Kamwe zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao.

Amesema, “Nathibitisha tunamshikilia Msemaji wa Yanga, Ali kamwe tunamshutumu kwa kutoa kauli mbaya dhidi ya viongozi wa Serikali, tunaendelea na mahijiano nae na tutatoa taarifa.”


