Zaidi ya Wakazi 300 mkoani Shinyanga wamejitokeza kupima kwa hiari magonjwa yasiyoambukiza ambapo 28 kati yao wamethibitishwa kuwa na kisukari, 78 uzito uliopitiliza, shinikizo la damu 100, idadi inayopelekea ugonjwa huo kuongoza kushika kasi zaidi.
Daktari idara ya magonjwa ya ndani Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Shinyanga Emmanuel Sadiki ameeleza hayo leo wakati akizungumza na Jamo Fm ikiwa ni siku ya mwisho ya wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza hospitalini hapo yaliyoanza novemba 13 na kutamatika leo Nov 17, 2023.
Dr. sadiki amesema kuwa kundi lililothibitishwa kuwa na shinikizo la damu ya juu ni kati ya umri wa miaka 40 mpaka 60 na wachache walio chini ya miaka 30 mpaka 35.
Pamoja na hayo Dokta Sadiki amesisitiza wananchi kuendelea kujitokeza na kuwa na desturi ya kwenda hospitali kufanya vipimo mara kwa mara ili kuepukana na magonjwa ya namna hiyo haswa pressure ambayo kwa kiasi kikubwa husababisha magonjwa mengine ikiwemo figo, moyo na kiharusi.