Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Kati ya watoto 100,000 kuna watoto 50,000 wamedumaa

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amesema viongozi wa Mkoa huo wapo tayari kuondolewa madarakani iwapo watashindwa kumaliza changamoto ya udumavu na utapiamlo, ambapo takwimu za mkoa huo zinaonesha katika watoto wenye umri chini ya miaka mitano zaidi ya 100,000, watoto zaidi ya 50,000 wamedumaa.

Mtaka amesema hayo katika kikao cha wadau wa lishe ambapo amesema kama kutakuwepo na mipango na ufuatiliaji wa mipango hiyo na ushirikiano wa dhati kwa kiwango cha wakazi wa mkoa huu 800,000 hakiwezi kuwashinda kushughulikia changamoto hiyo.

Aidha, Mtaka amewataka viongozi wanawake waliopo ndani ya mkoa huo kujiunga kwa pamoja na kuwa mstari wa mbele kushughulikia suala la udumavu kwa uzito na uharaka kwa sababu wana nafasi kubwa ya kukutana na wanawake wenzao na kuzungumza nao kwa ufasaha.

Amewataka maafisa Afya kuainisha maeneo sahihi yenye udumavu na utapiamlo kwa kiwango kikubwa ndani ya Mkoa ili kurahisisha mikakati ya kushughulikia ikihusisha viongozi wa vijiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *