
Na Daniel Gahu – Katavi
Mkoa wa Katavi umeandaa tamasha kubwa la Samia Day ili kutangaza Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Julai 4, hadi 05, 2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Inyonga Wilayani Mlele.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi ndugu Albert Msovera amesema lengo la tamasha hilo ni kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais Kwa mchango wake wa kuleta fedha nyingi ambazo ni zaidi ya Trilioni Moja nukta tatu ambazo zimesaidia kutekelezwa Kwa miradi mingi ya maendeleo Mkoani Katavi.
Pia amebainisha kaulimbiu ya tamasha hilo kuwa ni “Asante Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa fedha za maendeleo, “Katavi Imara na Maendeleo Imara”. Ambapo wahusika wakuu wa tamasha hilo ni Serikali ya Mkoa, taasisi zote na kushirikiana na TIMU KIZIMKAZI.
Aidha, tamasha hilo litaambatana na burudani mbalimbali, matembezi ya hiyari pamoja na kutembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi Kwa lengo la kutembelea na kujifunza vyanzo vya utalii katika mbuga hiyo iliyopo ndani ya Mkoa wa Katavi .
Akihitimisha kuzungumza mbele ya waandishi wa habari, ndugu Msovera amesema kilele Cha tamasha hilo itakuwa ni July 5 na kuwaomba wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kujitokeza Kwa wingi ili waadhimishe Kwa pamoja mafanikio yakimaendeleo yaliyofanyika ndani ya Mkoa kutokana fedha alizotoa Mheshimiwa Rais.