
NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA
HATIMAE mchakato wa kura za maoni, jimbo la Shinyanga mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) umefika tamati ambapo mbunge wa jimbo hilo aliyemaliza muda wake Patrobas Katambi ameibuka kidedea kwa kupata kura kura 2,922 kati kura 3930 zilizopigwa huku kura 32 zikiharibika na kusaliwa na kura halali 3898.
Wengine walioshiriki mchakato huo wa kuomba ridhaa ya chama hicho kuogombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ni pamoja na Stephen Masele aliyepata kura 874, na Paul Brand akipata kura 34,lakini pia Abobuakar Mukadamu amepata kura 25na hassan Fatihu akiibuka na kura 25,naye Hosea Karume amepata kura 16 huku Eustard Ngatale akiibuka na kura 10.

Akizungumza mara baada ya kutangaza matokeo hayo katibu wa wilaya ya Shinyanga wa chama cha mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mkurugenzi wa uchaguzi Hamisa Chacha amesema hayo ni matokeo ya awali vikao ndani ya chama hicho bado vinaendela ili kumpta mtu atakayepeperusha bendera ya chama hicho na kuwataka wagombea wote kuwa watulivu kusubiri maamuzi ya chama hicho.
Naye mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini Anord Makombe amesema uchaguzi ndani ya chama hicho umefanyika kwa uwazi na demokrasia ya hali ya juu huku akiwapongeza wagombea ambao kura zao hazikutosha lakini wamekubali kusaini matokeo hayo kusubiri maamuzi ya chama
“Napenda kuwapongeza sana wagombea wote hata wale ambao kura zao hazikutosha lakini wamekubaliana na matokeo na kusaini hiyo ndiyo demokrasia “amesema Makombe


