Na Eunice Kanumba – Shinyanga
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi amesoma na kuielezea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020/2024, kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM jimbo la Shinyanga Mjini na Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi.
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu, amesema utekelezaji umefanyika kwa kipindi cha miaka minne tangu achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga huku akianisha kuitekeleza kwa asilimia 100
ELIMU.
Amesema, ndani ya miaka minne kipindi anaingia kwenye ubunge kulikuwa na upungufu wa madarasa 4, lakini zimejengwa shule mpya 9,msingi shule 5 na sekondari 4.
Pia amefanikisha kuwepo na tawi la chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo hapa Shinyanga, upanuzi chuo kikuu cha Moshi (Mucops) tawi la Kizumbi.
MIUNDOMBINU.
Kwa kipindi chake umejengwa uwanja wa ndege wa Ibadakuli, ameboresha miundombinu ya barabara, madaraja ambayo yalikuwa korofi, likiwamo la Uzogole, Iwelyangula, Ibinzamata, Kitangili,Ndala,Ihapa,Mwamalili,na Ndembezi Mwanoni.
Amemuomba pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Ally Hapi kusukuma suala la ujenzi wa barabara ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza.
Amesema pia katika uboreshaji wa miundombinu hiyo wapeta tena fedha za ujenzi wa stend mpya, Soko kuu, ambapo pia ameboresha masoko mengine ilikiwamo la Ngokolo Mitumbani,Ibinzamata,Majengo mapya, stendi ya Kambarage,Maegesho ya Magari, na eneo la mapunziko Nbc na kukarabati ya stend ya Manyoni.
AFYA
Ameboresha miundombinu ya afya kikiwamo kituo cha Afya Kambarage,Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga,Hospitali ya Rufaa,ujenzi wa Zahanati 6 na Vituo vya Afya kikiwamo cha Ihapa.
Amesema pia ametoa Ambulance zaidi ya 6 ambazo alipewa na Rais Samia Suluhu Hassan, ili kuboresha usafiri kwa wagonjwa.
MAJI
Amesema wameongeza mtandao wa maji kwa wananchi wengi na kusambazwa pia katika maeneo ya Bugwandege, Masekelo, Mwamasheke, Mwanubi, Busongo na maeneo ya mjini, na kwamba amepokea sh.bilioni 195 kwa ajili ya usambazaji wa maji jimboni na mradi utaanza kipindi hiki cha 2024/2025.
MIKOPO.
Amesema kwa upande wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga jumla ya sh.miliioni 200 imetolewa kwa vikundi 34 vya Boda boda,Bajaji na Vikundi vya akina Mama na watu wenye ulemavu, pi sh.milioni 19 imetolewa ya mikopo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu.
UMEME
Amesema maeneo mengi yameunganishwa na huduma za umeme.
MAPATO
Amesema kwa kipindi chake cha Ubunge ameongeza ukusanyaji mapato kutoka sh.milioni 800,bilioni 1 hadi sh.bilioni 5.
NISHATI SAFI YA KUPIKIA
Amesema, amegawa mitungi ya gesi 1,780 kwa makundi mbalimbali ya wananchi ili kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za matumizi ya Nishati safi ya kupikia.
MICHEZO.
Katambi amesema kuwa amekuwa akisaport michezo na hata kuanzisha ligi mbalimbali ilikuibua pia vipaji vya vijana,huku akitoa zawadi nono kwa washindi wa kwanza hadi sh.milioni 6.
UJENZI WA CHAMA
Amesema amejenga Ofisi za Chama,ikiwamo ya Ibadakuli sh.milioni 54 pamoja na Chibe yenye thamani ya sh.milioni 48.
Aidha,amewaomba wanaCCM kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na kwamba hakuna haja ya kugombana na kwamba adui wao mkubwa iwe ni maeneo ambayo hayana maendeleo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Odilia Batimayo amempongeza Mbunge Katambi kwa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM,huku akimtaka apige kazi na kuonya watu ambao wamekuwa wakivunja kanuni na maadili ya Chama hicho na kuanza kufanya kampeni za kugombea Ubunge kabla ya wakati.
“Acheni Mbunge ambaye bado yupo Madarakani afanye kazi, msipige Kampeni kabla ya wakati hata Mwenyekiti wetu Taifa ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan ameonya hilo na mimi nitaendelea kusimamia nidamu ya Chama,” amesema Odilia.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi, amempongeza Mbunge Katambi kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo, hali ambayo inajenga imani ya Chama kwa wananchi na hata kukipatia ushindi kwenye uchaguzi Mkuu.
Amewataka Wabunge pamoja na Madiwani kuendelea kuchapa kazi na kukamilisha ahadi ambazo waliahidi wananchi na kuacha kukatishwa tamaa na watu wanawania nafasi zao,huku akimsisitiza Katibu wa CCM kuendelea kudhibiti nidhamu za watu ambao wanapiga kampeni kabla ya wakati.
Aidha, amewatahadharisha watu ambao wameanza kampeni za mapema kwamba wajihadhari na Madalali wa kisiasa katika kipindi hiki cha uchaguzi, sababu ndiyo muda wao wa mavuno na watawapeleka pabaya kufuatia maadili ya chama kuwazuia kufanya hivyo.
Amesema uchaguzi wa mwaka huu ni wakujipanga na kila mtu atabebwa na kazi ambazo amezifanya na siyo kuanza kupanga safu ya wajumbe sababu Rais Samia tayari ameshachana mikeka yao, huku pia TAKUKURU itakuwa kazini kwenye changuzi ndani ya chama ya kutafuta Wabunge na Madiwani ambao watasimama kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi Mkuu.
Amesema wakati wa kampeni viongozi pamoja na wagombea wanapaswa kuelezea mambo ambayo yamefanywa ya utekelezaji wa Ilani kwa wananchi ili wapate ushindi wa kishindo kutokana na kufanya siasa za kisayansi na kujenga hoja.
Aidha,katika usomaji huo wa utekelezaji wa ilani, pia Mbunge Katambi alitoa kiti mwendo kwa mtoto mwenye ulemavu Delfina Mashaka ambacho kilikabidhiwa na Katibu Jumuiya ya wazazi CCM Taifa Ally Hapi, pamoja na kukabidhi Spika 4 na Maiki 4 kwa uongozi wa Stendi ya Mabasi ya Mkoani.