Rapa Kanye West kutoka nchini Marekani, amejitokeza hadharani na kuichana kampuni ya Adidas kwa kuuza “Yeezy 350s fake”.
Katika post aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram jana Februari 26, Kanye amefunguka kwa kusema yeye kupitia kampuni yake hawajawahi kutengenza Yeezy za rangi hizo hivyo wanachofanya Adidas ni kumkosea yeye na kuikosea biashara yake hiyo na ilihali wanamshitaki.
“Mtu yoyote anayependa Ye, hawezi kununua Yeezy Fake, sijawahi kutengenza viatu vya rangi hii, na pia silipwi kabisa na Adidas ila wamenishitaki,” ameandika Kanye