Sio kwa amefulia bali ni maamuzi tu ambayo amefanya rapa Kanye West kwa kuuza nyumba yake ya kifahari huko Malibu, California nchini Marekani na anauza kwa kiasi cha Dola Milioni 53 sawa na Tsh.Bilioni 132.5 .
Nyumba hiyo ya Kanye aliinunua mwaka 2021 kwa kiasi cha Dola Milionin 57, ambayo sawa na Tsh. Bilioni 142.2.
Ila angalizo nyumba hiyo tangu imenunuliwa imekuwa ikikarabatiwa tu na mpaka sasa bado haijamaliza ukarabati hivyo unaweza kumalizia mwenyewe ukarabati.