KANISA LA GWAJIMA LAIOMBA MAHAKAMA KUONDOA ZUIO LA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE

Kupitia Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church maarufu kwa jina la Ufufuo na uzima, limefungua kesi ya kuomba amri ya muda ya kuondoa zuio la kuendelea na shughuli zake, ili kulinda hadhi ya usajili.

Kanisa hilo, ambalo linaloongozwa na Askofu na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Josephat Gwajima lilifungwa hivi karibuni na Serikali, kwa tuhuma za kutumika kisiasa, kitu ambacho ni kinyume na leseni ya usajili.

Anayewakilisha kesi hiyo ni Wakili Peter Kibatala ambaye amesema shauri hilo namba 13189 la mwaka 2025 limefunguliwa dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Taasisi za Kiraia.

Wanaitaka Mahakama kuondoa zuio la kufungiwa kwa Kanisa hilo wakati Rufaa iliyokatwa na Kanisa hilo kupinga kuzuiwa kufanya shughuli zake za kidini, ikifanyiwa kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *