Kampuni Zaidi ya 50, Wajasiriamali Kushiriki Maonesho Geita

Kampuni zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali duniani pamoja na wajasiriamali zaidi ya 100 wanatarajiwa kushiriki maonesho ya Wakandarasi, Wahandisi na Sekta ya Ujenzi Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita chini ya Udhamini wa Kampuni ya Jambo Group.

Maandalizi ya Kushiriki Maonesho ya Wakandarasi, Wahandisi na Sekta ya Ujenzi Mkoani Geita yakiendelea na hapa ni shughuli za Ujenzi wa Banda la Bidhaa za Jambo Group of Companies katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.

Maonesho hayo yameanza leo April 18 yakitarajiwa kutamatika April 28 na yamelenga zaidi kutoa elimu pamoja na kubadilishana ujuzi juu maswala ya ukandarasi pamoja na Ujenzi na Mwenyekiti wake George Mandia amesema yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Geita na yanatarajiwa kwa kiasi kikubwa kusaidia kuinua uchumi wa wakazi wa Mkoa huo na kuwaunganisha pamoja Wakandarasi, Wahandisi na sekta ya Ujenzi kwa ujumla Tanzania.

Moja kati ya Mashine zinazotumika katika Shughuli za Ujenzi kama inavyoonekana ikiwa katika Viwanja vya maonesho ya Wakandarasi, Wahandisi na Sekta ya Ujenzi Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.

Nao Baadhi ya washiriki pamoja na wadau waliojitokeza katika maonesho hayo wamesema yatasaidia kwa kiasi kikubwa kutangaza teknolojia mpya za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali hali ambayo itawasaidia wajasariamali waliojitokeza katika maonesho kutumia teknolojia hizo kujiinua kiuchumi.

Mashine mbalimbali za kusaga na kukoboa zilizopamba siku ya kwanza ya ufunguzi wa Maonesho ya Wakandarasi, Wahandisi na Sekta ya Ujenzi Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *