Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Shinyanga Oktoba 11, 2025, kufanya mikutano ya kampeni akiomba ridhaa ya wananchi ili waweze kumchagua.
Akizungumza na Jambo Media, Katibu wa Itikadi, Siasa, Uenezi na Mafunzo (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Richard Masele amesema Dkt. Samia anatarajiwa kuwasili na kupokelewa majira ya asubuhi ambapo akiwa njiani kuja Shinyanga atawasaliamia wananchi wa Kata ya Maganzo, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.

Amesema, katika mkutano Dkt. Samia ataelezea miradi yote mikubwa na kimkakati aliyotekeleza katika mkoa wa Shinyanga katika kipindi cha miaka minne aliyokuwa madarakani, lakini pia ataainisha yale anayotarajia kuyafanya katika kipindi cha 2025/2030 endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa.
Baada ya mkutano huo Dkt. Samia anatarajiwa kuendelea na ziara yake Manispaa ya Kahama kwa kufanya mkutano mwingine wa hadhara.


