Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unatarajia kufunga Kamera katika eneo la Kibiashara Kariakoo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ufanyaji wa biashara kwa saa 24 na udhibiti wizi na uhalifu .
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hii leo Februari 18, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema lengo la mpango huo pia ni kuimarisha usalama wa Wananchi na wafanyabiashara.

Amesema, upango huo utagharimu jumla ya shilingi milioni 514 ambapo kwa kuanzia jumla ya kamera 40 zitakazofanya kazi kwa saa 24 zitafungwa katika awamu ya kwanza.
Kariakoo ni kitovu kikubwa cha biashara katika Afrika Mashariki ya Kati na kwingineko, na ufungaji wa Kamera hizo zitasaidia kurahisisha utambuzi wa matukio, kuimarisha ufuatiliaji wa wahalifu na kutoa ushahidi wa haraka.