Na Eunice Kanumba – Shinyanga.
Kambarage vijana kwaya (KVC) inayohudumu katika kanisa la African Inland Church (AICT) la mjini Shinyanga leo tarehe 22 August 2026 wamezindua rasmi maandalizi ya ibada ya mkesha wa tukio la nimebeba ushuhuda unaotarajiwa kufanyika kiwanja cha kanisa la AICT Shinyanga katika eneo la Kambarage manispaa ya Shinyanga wenye lengo la kumtangaza Yesu kristo , kuliombea Amani taifa la Tanzania pamoja na kurekodi mubashara nyimbo za kwaya hiyo.
Mkesha wa ibada hiyo unatarajiwa kufanyika Oktoba 16, 2026 katika Kanisa la AICT Kambarage, lililopo Manispaa ya Shinyanga, kwa udhamini wa jambo fm pamoja na wadau wengine huku wananchi Zaidi ya 3000 wakitarajiwa kuhudhuria tukio hilo.

Akizungumza leo, Agosti 22, 2026, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Vigimark uliopo Mjini Shinyanga, Mwenyekiti wa kwaya hiyo , Heri Ndaki, amesema ibada ya mkesha huo ni makutano katika kumwadhimisha Mungu, pamoja na kuomba Amani iliyoasisiswa na viongozi wa taifa letu akiwemo mwalimu Julius Kambarage Nyerere iendelee na pasiwepo na machafuko ambayo yamewakumba baadhi ya mataifa hapa dumiani.
Amesema ni muhimu kwa viongozi wa dini na waumini kutoka madhehebu mbalimbali kuendelea kuungana katika kuliombea Taifa na kuhamasisha amani, upendo na mshikamano ndani ya jamii.

Naye Mchungaji wa Kanisa la AICT Kambarage, Mapambano Jacob, amesema kanisa limeendelea kuwalea vijana na kwamba vijana wamekuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa taifa hivyo kanisa limeendelea kuwalea katika misingi ya kumjua mwenyezi Mungu ili kuwa na taaifa lenye maadili na kumjua mwenyezi Mungu.
Naye Mwenyekiti wa hamasa katika kwaya hiyo John Mathias sambamba na jambo fm ameanisha pia wadau wengine walioshirikiana katika kufanikisha ibada hiyo kuwa ni pamoja na chuo cha sayansi za afya Kolandoto pamoja na hotel ya Vigimark iliyopo katika manispaa ya Shinyanga huku akiwataka wadau wengine kujitokeza kufadhili ibada hiyo ili kazi ya Mungu iweze kufanikiwa.

Aidha Mwenyekiti wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa kwaya hiyo Reuben Emmanuel, amesema tamasha hilo litakuwa na uimbaji mubashara wa nyimbo zote 15 zinazounda albamu ya Nimebeba Ushuhuda na kuanisha mavazi na chapa zikazotumika katika mkesha wa ibada hiyo na kwamba kutakuwa na tshirt zitakazouzwa kuanzia shilingi 10000 za watoto, huku za wakubwa zikiwa ni shilingi 15000 za mikono mifupi pamoja na 25000 zile za mikono mirefu.
Ameomba wadau mbalimbali kuendelea kuunga mkono maandalizi ya tamasha hilo kwa kuchangia kupitia M-Pesa namba 58130016 au akaunti ya CRDB, AIC KVC Maendeleo, namba 0133583913800.

Wadau wanaotaka kupata maelezo zaidi kuhusu tamasha hilo wanaweza kuwasiliana na uongozi wa kwaya hiyo kupitia namba 0752-265721 au 0627-265721.


